| |
| | TANZANET - Diwani ya Tanzanet |
 | | Azma ya Diwani ya Tanzanet ni kuhamasisha Watanzania na Watumiaji wote wa lugha ya Kiswahili kujaribu kutunga, kueleza mambo mbali mbali kwa lugha fasaha, kishahiri, ikiwa pamoja na kueleza mambo mbali mbali yanayomhusu Matanzania na mazingira yake yaliolezwa kiasanii. |
 | | Diwani ya Tanzanet itaweza kufikisha tenzi, tungo, na mashiri mbali mbali kwa uwanja mpana zaidi ambao utasaidia kupanua mawazo na ufahsaha wa lugha na jinsi ya kuitumia kwa kufupisha maana iliyoelezwa katika sehemu mbali mbali wakati huo huo kufikisha ujumbe rasmi, bila kupoteza maana yake. |
 | | Diwani ya Tanzanet itakuwa uwanja wa kutoa mawaidha, mafumbo, kumueleza mtu sifa na tabia zake, kutabili hali ya wakati, kuonya, na kutoa mwanya kwa malumbano ya kishahiri. |
| tanzanet.org /int/diwani/index.html (184 words) |
|