| |
| | Wengi wajitokeza kushiriki Kili Marathon |
 | | Akizungumza na waandishi wa habari jana kwenye ukumbi wa Idara ya habari Maelezo, meneja uhusiano wa TBL Aggrey Marealle, alisema mashindano hayo yatashirikisha nchi za Afrika Kusini, Uholanzi, Marekani, Sweden, Uganda, Kenya, Namibia, Zimbabwe Ufaransa, Uingereza na wenyeji Tanzania. |
 | | “Tuna zaidi ya wageni 160, wamejitokeza katika kushiriki mbio hizo, Sweden watashiriki kwa mara ya kwanza” alisema Marealle. |
 | | “Mwaka huu tumeongeza zawadi kwa washindi wa mbio hizo—wanawake na wanaume kila mmoja atapata shilingi milioni 1.5” alisema Marealle. |
| www.ipp.co.tz /ipp/nipashe/2004/02/10/5341.html (216 words) |
|